Ijumaa, 1 Novemba 2013

Kolo Toure apania kuwaonyesha kazi Arsenal


BEKI wa kati wa Liverpool, Kolo Toure amesema amepania kuwakomesha Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu England utakaofanyika Jumamosi ijayo ili wajutie makosa yao ya kumuacha. Kolo anatarajia kuwamo kwenye kikosi cha Liverpool kitakachoifuata Arsenal kwao na beki huyo wa Ivory Coast amepania kumtibua zaidi kocha Arsene Wenger.
“Ni pale nilipoanza kucheza mpira hapa England. Wao walinipa nafasi ya kuja hapa,” alisema Kolo.
“Siku zote ni kitu kizuri kwangu kucheza dhidi yao, lakini nilichokipanga nataka kuwaonyesha kwamba walifanya makosa kuniacha.
“Naamini mechi hiyo itakuwa nzuri kwangu kwa sababu siku zote mambo yamekuwa safi ninapocheza dhidi ya klabu nilizowahi kuzichezea. Ninajitahidi kwa uwezo wangu wote kuwaonyesha kwamba mimi ni mchezaji mahiri. Lakini, kubwa ni kuisaidia timu yangu.”
Kolo Toure aliondoka Arsenal na kujiunga Manchester City mwaka 2009. Wakati huohuo, kambi ya Arsenal imepata faraja baada ya straika wake Lukas Podolski kurejea na kufanya mazoezi katika kikosi cha kwanzaposted by king spot.blogspot.com
.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni